Maonyesho hayo yamepangwa kuendelea hadi Alkhamisi ijayo ya tarehe 16 Februari. Maonyesho hayo yanafanyika kwa msaada wa Saud bin Saqr Qassimi, mwanachama wa Baraza Kuu la Watawala wa Ras al-Khaima na Faisal bin Saqr Qassimi, Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Fedha cha Zawadi ya Qur'ani ya Ra's al-Khaima.
Baada ya kufunguliwa maonyesho hayo, Faisal bin Saqr Qassimi alitembelea vitengo vinavyoonyesha nakala na picha za maandishi ya mkono ya Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu na vilevile picha zinazohusiana na taasisi za Qur'ani za Imarati. Ametembelea pia vitengo vinavyohusiana na nakala za kale kabisa za Qur'ani Tukufu, nakala ambazo ziliandikwa katika karne ya tano hijiria.
Amesema wakati wa kutembelea maonyesho hayo kwamba lengo kuu la kuandaliwa maonyesho hayo ni kueneza taaluma na maarifa ya Qur'ani Tukufu miongoni mwa watu pamoja na kuwafahamisha mbinu na zana zinazotumika kwa ajili ya kuhifadhi Qura'ni katika nchi mbalimbali za dunia. 951147