Benki hiyo ijulikanayo kama Benki ya Amana imezinduliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Tanzania Mh. Saada Mkuya Salum akiwa ameandamana na wakurugenzi wa benki hiyo Dr Idriss Rashid na Bw. Haroon Pirmohamed.
Benki hiyo ambayo imekuwa ikiendesha shughuli zake kwa mwaka mmoja sasa inajivunia kuwa benki ya kwanza kabisa ya Kiislamu nchini Tanzania.
Wakurugenzi wa benki hiyo wanasema lengo kuu la kuanzishwa taasisi hiyo ya kifedha ni kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee ambazo zinafuata Sharia za Kiislamu kikamilifu kwa kuzingatia maadili na kwa njia iliyowazi na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wateja.
Mbali na akaunti kadhaa za kawaida banki hiyo pia imeanzisha akaunti maalumu ya akiba kwa ajili ya wanaotaka kutekeleza ibada ya Hija.
1145912
2 : ni mwenyekiti wa asasi inayosaidia yatima, wagojwa na familia fukara.
Je ! Kuna fungu kwa ajili ya wahitaji?
Kama lipo naomba mawasiliano ya mkuu wa kitengo.