IQNA

Jeshi la Iran lanasa ndege ya kijasusi ya Marekani

16:20 - December 04, 2012
Habari ID: 2458517
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran limefanikiwa kukamata ndege ya kijasusi ya Marekani isiyo na rubani baada tu ya kuingia kinyemela katika anga ya Iran.
'Drone' hiyo ijulikanayo kwa jina la Scan-Eagle inasemekana kuwa na teknolojia ya kisasa zaidi ya kuweza kuepuka rada lakini jeshi la Iran limeweza kugundua ndege hiyo isiyo na rubani.
Wataalamu wa masuala ya kijeshi wamesema kuwa, Iran imeonyesha ustadi mkubwa kwa kuinasa ndege hiyo ya kijasusi na kwamba hiyo ni kengele ya hatari kwa Marekani kwamba uwezo wa kijeshi wa Iran ni mkubwa kuliko wanavyodhania.
Yapata mwaka mmoja uliopita pia jeshi la Iran lilifanikiwa kushusha chini kitaalamu ndege nyingine ya Marekani isiyo na rubani baada ya kuingia katika anga ya Iran bila idhini.
Huku hayo yakijiri, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ramin Mehmanparast amekosoa njama mpya ya kuiwekea Iran vikwazo vipya akisema si mashinikizo wala vikwazo hivyo vitaipigisha magoti serikali ya Iran na kwamba mashinikizo na vikwazo hivyo ni kinyume cha sheria. 1148206
captcha