Kituo cha habari cha France24 kimeripoti kuwa, kundi moja la watengeneza filamu wa Denmark limetengeneza filamu mpya ambayo inakebehi na kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu, suala ambalo limezusha hasira za Waislamu.
Denmark imekuwa ikitumia vibaya uhuru wa kusema na kujieleza kwa ajili ya kutengeneza na kurusha hewani filamu zinazovunjia heshima matukufu ya Kiislamu hususan Mtume Muhammad (saw).
Watengenezaji wa filamu hii mpya ni watu wenye misimao ya kufurutu mipaka wanaofanya jitihada za kufanyia istihzai na kebehi mafundisho ya Uislamu.
Waislamu wa Denmark wamepinga vikali filamu hiyo na wamewataka viongozi wa serikali ya nchi hiyo kuwafikisha mahakamani watengenezaji wake. 1188428