Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran, Ayatullah Ahmad Khatami amesema leo kuwa, pendekezo la Marekani la kutaka kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mtego uliogunduliwa kitambo sio tu na Tehran pekee bali pia na wapenda haki na uadilifu kote duniani.
Ayatullah Khatami amesema Washington haikuwa na nia njema ilipotoa pendekezo hilo. Amesema Wamarekani hawana nia ya mazungumzo ya kweli. amesema kuwa engo lao ni kutaka kuionyesha dunia kwamba wanaweza kuwaburuza wanamapinduzi shupavu wa Iran kwenye meza ya mazungumzo na kuongeza kuwa Tehran inaujua ujanja huo na ulimwengu mzima unautambua
Khatibu wa muda wa Sala ya Ijumaa hapa mjini Tehran aidha amezungumzia kadhia ya Syria, Palestina na Bahrain. Kuhusu Syria, Ayatullah Khatami amesema njama za Wamagharibi za kutaka kuiangusha serikali halali ya nchi hiyo zimegonga mwamba na kwamba njia pekee ya kutatua mvutano ulioko ni mazungumzo kati ya serikali na wapinzani pasina kushinikizwa au kuingiliwa na wageni. Amelaani kitendo cha nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani cha kuwapa silaha magaidi kwa lengo la kuipindua serikali ya Rais Bashar Asad. 1186213