Kituo cha bahari cha al Masrawi kimetangaza kuwa, al Baradei ambaye alikuwa akizungumza na watu wanaofanya mgomo wa kuketi chini katika Wizara ya Utamaduni ya Misri ameashiria matamshi yaliyotolewa na baadhi ya watu walioshiriki kwenye mkutano wa Masalafi Jumamosi iliyopita katika uwanja wa mpira wa Cairo chini ya usimamizi wa Rais Muhammad Mursi wa Misri na kusisitiza kuwa, wakati utawala unapoketi na kusikiliza matamshi ya watu wanaowaita Waislamu wa madhehebu ya Shia kuwa ni najisi na kuwadunisha wapinzani, suala hilo linasisitiza kuwa utawala huo haupaswa kubakia madarakani hata siku moja.
Al Baradei ameongeza kuwa, mapinduzi ya wananchi wa Misri yametokomezwa na kwamba Wamisri wanapaswa kumiminika tena mitaani tarehe 30 Juni kwa ajili ya kudumisha mapinduzi yao.
Ikumbukwe kuwa katika mkutano wa kundi la Masalafi uliofanyika Jumamosi iliyopita katika uwanja wa mpira wa Cairo chini ya uongozi wa Rais Muhammad Mursi wa Misri ambapo mmoja kati ya maulamaa wa kundi hilo aliwahujumu Waislamu wa madhehebu ya Shia na harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Katika mkutano huo Mursi alitangaza habari ya kukatwa uhusiano wa Misri na Syria. 1244248