Ripoti ya kamati hiyo imesema kuwa jeshi la Israel linawatesa watoto wadogo linaowachukua mateka wa Kipalestina na kuwatumia kama ngao ya kibinadamu katika operesheni zake za kijeshi.
Ripoti hiyo imesema Israel hairuhusu kusajiliwa majina ya watoto wanaozaliwa Gaza au Ukanda wa wa Magharibi na unawanyima huduma muhimu za afya, tiba, maji ya kunywa na elimu.
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa watoto wa kipalestina wanaokamatwa na polisi na jeshi la Israel hulengwa kwa miamala mibaya na ya kudhalilisha na wengi wao huteswa. "Watoto hao husailiwa kwa lugha ya Kiebrania ambayo hawaielewi na hulazimishwa kusaini fomu zilizoandikwa kwa lugha hiyo ambazo kwa hakika huwa zina maandiko ya kukiri makosa ambayo hawajafanya", imesisitiza ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa.
Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa watoto wengi wa Kipalestina hutiwa nguvuni kwa kosa la kurusha mawe na adhabu ya kosa hilo huwa kifungo cha miaka 20 jela! 1246252