Waislamu wa madhehebu ya Shia katika maeneo mbalimbali duniani jana tarehe 8 Shawwal walikumba tukio chungu la kuvunjwa na kubomolewa makaburi ya watoto, wajukuu, wake na masabaha wa Mtume (saw) huko Baqii katika mji mtakatifu wa Madina.
Makaburi ya Baqii ambayo yanajumuisha makaburi ya Ahlul Bait wa Mtume (saw) yaani Imam Hassan al Mujtabaa (as), Imam Zainul Abidin (as), Imam Muhammad al Baqir na Imam Sajjad (as), na vilevile mama wa Imam Ali bin Abi Twalib Fatima binti Asad (as) na mamia ya masahaba wa Mtume, yaliharibiwa na Mawahabi wa Saudi Arabia tarehe 8 Shawwal mwaka 1343 Hijria.
Mawahabi wa Saudia pia walitaka kuvunja kaburi tukufu la Mtume wetu Muhammad (saw) lakini maandamano na upinzani mkubwa uliofanywa na Waislamu katika maeneo mbalimbali uliwazuia kutimiza lengo lao la kishetani. 1273748