IQNA

Sheikh wa al Azhar alaani shambulizi dhidi ya kanisa

17:08 - October 21, 2013
Habari ID: 2606658
Sheikh Mkuu wa al al Azhar nchini Misri amelaani vikali shambulizi la kigaidi lililofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya kanisa la al Adh'raa katika wilaya ya Giza.
Taarifa iliyotolewa na Sheikh Ahmad al Tayyib imesema, shambulizi la kigaidi lililolenga Kanisa la al Adh'raa wilayani Giza ni kitendo cha jinai kinachopingana na dini na maadili.
Mufti wa Misri Shauqi Allam pia ametoa taarifa akilaani shambulizi hilo na kutangaza kuwa, dini ya Uislamu inaharamisha na kukataza kuvunjiwa heshima au kuharibiwa makanisa, kulipua mabomu na kuua watu wanaokuwamo na kuzusha hali ya hofu baina ya wafuasi wa makanisa hayo.
Mufti wa Misri amewataka Waislamu na Wakristo wa Misri kushikamana kwa ajili ya kuzima fitina zinazoenezwa na baadhi ya watu nchini Misri.
Makundi mbalimbali ya kisiasa ya Misri pia yamelaani shambulizi lililofanywa na watu wasiojulikana dhidi ya Kanisa la al Adh'raa.
Watu wasiojulikana jana walishambulia Kanisa la Sayyida al Adh'raa katika wilaya ya Giza wakati Makopti walipokuwa wakitoka nje ya kanisa hilo na kuua watu wanne aliokuwa katika sherehe ya harusi. Watu wengine 18 walijeruhiwa. 1305939
captcha