IQNA

Sheria za Kiislamu kutekelezwa Brunei

21:30 - October 22, 2013
Habari ID: 2607291
Mfalme wa Brunei amesema sheria za Kiislamu zitaanza kutekelezwa katika mahakama za nchi hiyo hivi karibuni.
Sultan Hassanal Bolkiah wa Brunei amesema sheria za Kiislamu zitaanza kutekelezwa katika mahakama za nchi hiyo miezi sita ijayo. Amesema kuwa, utekelezaji wa sheria za Kiislamu nchini humo ni katika jitihada za kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa nchi ya Brunei iko kusini mashariki mwa Asia na mji mkuu wake ni Bandar Seri Begawan.
Jamii ya nchi hiyo ilikuwa watu laki nne mwaka 2001 na lugha yake rasmi ni Malai.
Dini rasmi ya Brunei ni Uislamu na zaidi ya silimia 60 ya watu wa nchi hiyo ni Waislamu. 1306425
captcha