Video iliyotolewa hivi karibuni imeonesha wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi wakilipua na kubomoa kwa mabuldoza misikiti kadhaa ya Waislamu wa Sunni na Haram tukufu za Mashia katika mkoa wa Salahuddin nchini Iraq.
Wakati huo huo magaidi hao wa Daesh wamelipua kanisa la kihistoria la St. George katika mji wa Mosul.
Katika siku za hivi karibuni jeshi la Iraq limepata mafanikio makubwa katika mapambano yake dhidi ya kundi hilo katika maeneo mengi ya nchi hiyo lakini bado vita vinaendelea dhidi ya kundi hilo lenye misimamo ya kufurutu ada.
Wanamgambo wa kundi hilo la kitakfiri na kigaidi wamekuwa wakifanya vitendo vya kikatili kama vile kuwakata vichwa na kuwasulubu watu wanaowakamata kutoka jamii mbalimbali za Iraq kama vile Mashia, Masunni, Wakurdi, Wakristo na jamii ya Wakurdi wa Izadi.../mh