Larijani ameyasema hayo katika hafla ya kufunga Mashindano ya Tano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Wanachuo Waislamu. Katika hotuba yake Larijani aliashiria uwezo mkubwa wa Waislamu duniani na kusema nchi za Kiislamu zinapaswa kutumia utajiri wao kuimarisha maisha ya Kiislamu kwa msingi wa Tauhidi.
Spika wa Majlisi ya Iran ameongeza kuwa kuzingatia mafundisho na misingi ya Qur'ani ndio nukta ya msingi katika maisha ya Mwislamu.
Larijani pia ameipongeza Taasisi ya Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti Iran kwa kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya wanafunzi wa vyuo vikuu .
Duru ya Tano ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya wanachuo Waislamu imefanyika Tehran kwa kuhudhuriwa na washiriki 66 kutoka nchi 57 duniani.
Washiriki hao ambao ni ni wanafunzi wa vyuo vikuu na walishindana kwa muda wa siku nne kusoma (qiraa) na kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika mnara wa Milad mjini Tehran.../mh
2671966