Hayo yamethibitishwa na Sheikh Ahmed el Tayeb, Sheikh Mkuu wa al Azhar Jumatatu alipokutana na Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi na kuongeza kuwa, chuo hicho kimeandaa kongamano hilo lengo likiwa ni kujadili na kutatua tofauti ndogo ndogo za kimitazamo zilizopo kati ya Waislamu wa madhehebu hayo mawili Kishia na Kisuni. Amesisitiza kuwa, hakupaswi kuwepo uadui hata kidogo baina ya umma wa Kiislamu hususan kati ya Kisuni na Kishia, hasa kwa kuzingatia kuwa kwa miaka mingi Waislamu hao wamekuwa wakiishi pamoja na kusaidiana. Ni vyema kuashiria hapa kwamba, baadhi ya mataifa ya eneo la Mashariki ya Kati kwa kushirikiana na madola ya Magharibi, yamekuwa yakichochea moto wa fitina na mifarakano kati ya madhehebu za Kiislamu kwa lengo la maslahi yao, moto ambao umepelekea kuibuliwa makundi ya kigaidi na kitakfiri ambayo yamekuwa yakifanya mauaji ya kutisha dhidi ya hata Waislamu.../