Waandamanaji hao walitoa nara dhidi ya gazeti hilo na kutaka kufukungwa balozi wa Ufaransa nchini Iran. Waandamanaji pia wamewataka maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuchukua hatua dhidi ya kitendo hicho cha kishenzi.
Maandamano kama hayo ya kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Mtume Mtukufu yameshuhudiwa pia katika nchi mbalimbalii duniani kama vile Somalia, Pakistan, Niger na Yemen.
Huko Chechniya makumi ya maelefu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Grozy kupinga hatua ya gazeti la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzi vinavyomkejeli Mtume SAW. Waandamaji hao walibeba mabango yaliyokuwa yameandikwa ‘Tunampenda Mtume Wetu.’