IQNA

Aghalabu ya misikiti CAR imeharibiwa

16:13 - March 18, 2015
Habari ID: 3008622
Ripoti zinasema kuwa karibu miskiti yote 436 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati imebomolewa kutokana na machafuko ya kidini.

Kwa mujibu wa Samantha Power mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa,  misikiti 417 kati ya misikiti yote ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imebomolewa tangu kuanza machafuko hayo zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Akiwa katika ziara ya ukaguzi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo alikitembelea kitongoji kimoja kilichosalia cha Waislamu katika mji mkuu Bangui, Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa aliwataja watu waishio mahala hapo kuwa ni "jamii iliyojawa na hofu kubwa." Samantha Power ameeleza wasiwasi kuhusu hali ya usalama ya Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya wanajeshi 750 wa Umoja wa Ulaya kuondoka nchini humo wiki iliyopita.../mh

3007496

captcha