Katika ujumbe wake huo, Dakta Ali Larijani Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Bunge la Iran linalipatia umuhimu mkubwa suala la maelewano na mazungumzo miongoni mwa nchi za Kiislamu. Amesema kwa njia hiyo ya maelewano kutapatikana ufumbuzi kwa matatizo yoyote yaliyopo baina ya nchi za Waislamu. Spika wa Bunge la Iran ameashiria aya ya Qur'ani Tukufu inayowataka Waislamu 'Washikamane na Kamba ya Allah SWT na wala wasifarakiane' na akasema Mtume SAW pia alisisitiza umoja, mshikamano sambamba na kukataza mifarakano baina ya Waislamu. Katika ujumbe wake huo Dakta Larijani ameongeza kuwa, matukio ya hivi karibuni katika ulimwengu wa Kiislamu ni ushahidi wa wazi kuhusu hatari ya kuenea fikra na utamaduni wa utumiaji mabavu wa matakfiri. Amesema tatizo la utakifiri ndio changamoto kubwa zaidi ya usalama na inayohatarisha umoja na ustawi wa Umma wa Kiislamu katika siku za usoni.
Kesho Alkhamisi 18 Juni imetangazwa kuwa siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1436 katika maeneo mengi duniani.../mh