Akizungumza wikendi hii wakati wa dhifa ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa wateja wake katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani huko Zanzibar, Mkuu wa Kitengo wa Mfumo wa Kiislamu wa Benki katika NBC, Nassir Masoud amesema wakaazi wa Zanzibar wana sababu ya kusherehekea.
Amesema kuanzishwa kitengo cha benki ya Kiislamu ndani ya NBC kumefanyika kwa misingi ya Kiislamu katika Qur’ani Tukufu.
Masoud ameongeza kuwa NBC ilianzisha huduma za Kiislamu miaka mitango iliyopita na hatua hiyo imewavutia wateja Zanzibar ambao walikuwa wanataka huduma za benki kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.../mh