Kundi la kigaidi ISIS au Daesh limetangaza kuhusika na hujuma hiyo ya Jumamosi katika mtaa wa al-Jeraf mjini Sanaa.
Wakati huo huo, wanajeshi wa Yemeni wakishirikiana na wapiganaji wa kamati za wananchi wameshambulia na kuharibu gari la jeshi vamizi la Saudi Arabia katika mji wa bandarini wa Aden. Kwa mujibu wa televisheni ya al-Masirah, wote waliokuwemo ndani ya gari hilo la deraya wamepoteza maisha walipokuwa wakijaribu kujipenyeza katika mji wa Aden.
Wakati huo huo ndege za kivita za Saudia zimeendeleza hujuma nchini Yemen ambapo katika tukio la hivi karibuni maeneo ya raia yamehujumiwa katika wilaya ya Harad mkoani Hajja. Mashambulio kama hayo yamefanyika pia jana katika mikoa ya Sa’ada na Amran.
Saudi Arabia ilianza kuishambulia kijeshi Yemen tangu tarehe 26 Machi, na hadi sasa watu zaidi ya 4,700 wameshauawa wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo.
Saudia imekiuka mapatano ya usitishwaji vita yaliyokuwa yameanza kutekelezwa wiki mbili zilizopita kupitia upatanishi wa Umoja wa Mataifa.
Saudia hata haiuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani bali iliendeleza mashambulizi yake dhidi ya watu wa Yemen katika mwezi huo mtukufu.../mh