IQNA

Naibu Mkuu wa Baraza la Mamufti wa Russia

Shughuli za Qur'ani za Jihadi vya Vyuo Vikuu ni fakhari kwa Waislamu

19:24 - September 05, 2015
Habari ID: 3358324
Sheikh Roushan Abbasov Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Mamufti wa Russia amesema shughuli na harakati za Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran ni chimbuko la fakhari kwa Umma wa Kiislamu kote duniani.

Mufti Abbasov Ameyasema hayo Jumatano mjini Moscow katika mkutano na Hamid Saber Farzam Mkurugenzi Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani la IQNA.
Katika kikao hicho Sheikh Abbasov alibainisha kuhusu harakati za Qur'ani nchini Russia ikiwa ni pamoja na mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini humo. Aidha alitoa wito kwa taasisi mbali mbali za Iran kuisaidia Russia katika kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qu'rani.
Sheikh Abbasov pia ametoa mwaliko kwa Iran kushiriki katika sherehe za uvunguzi wa msikiti mkubwa zaidi mjini Moscow. Sherehe hizo zinatazamiwa kufanyika Septemba 23 na kuhudhuriwa na wawakilishi wa nchi kadhaa. Naibu Mkuu wa Baraza la Mamufti wa Russia amesema amemtumia mwaliko Rais Hassan Rouhani wa Iran kushiriki katika ufunguzi wa msikiti huo wenye ghorofa saba.
Katika kikao hicho kumesisitizwa umuhimu wa kushirikiana zaidi katika uga wa habari za Qur'ani na ulazima kwa kuanzisha shirika la habari za Qur'ani kwa lugha ya Kirusi.
Kwa upande wake Hamid Saber Farzam Mkurugenzi Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani la IQNA amefafanulia Sheikh Abbasov kuhusu Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu nchini Iran. Taasisi hii inasimamia shughuli za IQNA.
Hamid Saber Farzam alikuwa safarini nchini Russia kuwakilisha IQNA katika Maonyesho ya 28 ya Vitabu Moscow.../mh

3357620

captcha