Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa baada ya kudhihiri athari mbaya za kushindwa Saudi Arabia kusimamia vyema masuala ya Hija utawala huo sasa unapaswa kuruhusu usimamizi wa ibada hiyo liwe suala la Kiislamu au uruhusu kuundwa kamati ya nchi za Kiislamu ya kusimamia na kuendesha masuala ya Hija.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amongeza kuwa Saudi Arabia imehusika na tukio la Mina na kwamba tuhuma zilizotolewa na viongozi wa nchi hiyo wakiwalaumu mahujaji kuwa ndio waliosababisha tukio hilo hazina msingi wowote.
Maelfu ya mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa Alkhamisi ya juzi wakitekeleza ibada ya Hija katika eneo la Mina umbali wa kilomita kadhaa kutoka Msikiti mtakatifu wa Makka.