Tovuti ya Morocco World News imeripoti kuwa, familia za Wamorocco hao wanashauriana na mawakili waandamizi katika masuala ya kimataifa kwa lengo la kuandaa mashtaka dhidi ya utawala wa Saudia katika mahakama za kimataifa. Wamorocco hao pia wamehoji kuhusu idadi kubwa ya mahujaji Wamorocco ambao hadi sasa hawajapatikana na kusema suala hilo limeshaanza kufuatiliwa na mawakili wao. Siku ya Ijumaa pia Wamorocco walifanya maandamano kulaani usimamizi mbovu wa Saudi Arabia katika ibada ya Hija. Wamorocco wanailaumu serikali ya Saudia kwa kutochukua hatua zozote za maana kuzuia maafa ya Mina. Hatua hiyo ya Wamorocco inachukuliwa huku idadi kubwa ya Waislamu duniani wakiendelea kuikosoa vikali serikali ya Saudia kwa usimamizi wake mbovu katika ibada ya Hija ambapo mwaka huu mnamo Septemba 24 maelfu ya mahujaji wameripotiwa kuaga dunia kufuatia msongamano mkubwa huko Mina.../mh