IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Uislamu ni dini ya amani, magaidi hawana uhusiano na Uislamu

20:16 - November 22, 2015
Habari ID: 3455805
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, jinai za kuogofya za makundi ya magaidi kama vile kukata vichwa na kuwachoma moto watu ni dalili ya kuwa mbali kabisa na Uislamu magaidi hao.

Aidha amesitiza kuwa Uislamu ni dini ya udugu, kupendana na kuwatakia wengine mema na kwa msingi huo jinai hizo hazina uhusiano wowote na Uislamu. Kiongozi Muadhamu ameyasema hayo leo hapa mjini Tehran alipokutana na rais wa Turkmenistan Gurbanguly Berdimuhamedow. Kiongozi Muadhamu amesema, katika kukabiliana na ugaidi na ukatili wa kundi la kigaidi la Daesh au ISIS na makundi mengine ya kitakfiri kama hilo ni kuwaruhusu watu watekeleze harakati sahihi za Kiislamu na njia bora ya kuzuia kuenea fikra za kigaidi ni kuimarisha fikra na misimamo ya wastani ya kihekima za Uislamu. Ayatullah Khamenei ameyataja mataifa ya Iran na Turkmenistan kuwa ni nchi mbili jirani na zenye udugu. Amesisitiza kuwa kuna udharura kwa nchi hizo mbili kuchukua hatua imara na za kivitendo za kutekeleza mapatano ya pande mbili. Kiongozi Muadhamu amesema Iran na Turkmenistan ni zenye mipaka ya amani na utulivu na hivyo Iran inaweza kutumiwa na Turkmenistan kama njia ya kufika katika Ghuba ya Uajemi. Kwa upande wake Rais wa Turkmenistan amebainisha furaha yake ya kukutana na Ayatullah Khamenei na kuongeza kuwa kufuata nasaha za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni jambo ambalo limekuwa na natija nzuri kwa nchi yake.../

3455793

captcha