IQNA

Barua ya Kiongozi imewasilisha mtazamo wa Kiislamu kuhusu ugaidi

19:36 - December 04, 2015
Habari ID: 3459723
Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa Gholam Ali Khoshrou amesema barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi iliwasilisha matazamo halisi wa Uislamu.

Akizungumza mbele ya kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya Alhamisi, Khoshrou alisema barua hiyo ililenga 'kuwasilisha kwa vijana mtazamo wa ndani wa Ulimwengu wa Kiislamu kuhusu vita dhidi ya ugaidi."
Khoshrou ametoa tamko hilo Alhamisi alipokuwa akihutubu katika kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambacho kilikuwa kikijadili 'Utamaduni wa Amani.' Katika kikao hicho Khoshrou amesoma baadhi ya sehemu za barua ya Kiongozi Muadhamu kwa vijana wa nchi za Magharibi.
Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi yaliyotokea Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita. Barua hiyo ambayo ni ya pili kwa vijana wa Magharibi baada ya ile ya Januari imeendelea kuakisiwa kote duniani huku wasomi na vijana wanaharakati wakisema imekuja wwakati unaofaa kwani kunaenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi pasina vijana wa nchi hizo kujua ukweli kuhusu Uislamu na Waislamu.

Kuisoma barua hiyo bonyeza hapa

3459696

captcha