IQNA

Rais Rouhani

Iran inataka kuimarisha umoja wa nchi za Kiislamu

10:45 - December 06, 2015
Habari ID: 3460265
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inataka kuchangia katika utulivu na maendeleo ya eneo la Mashariki ya Kati na kuimarisha umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inataka kuchangia katika utulivu na maendeleo ya eneo la Mashariki ya Kati na kuimarisha umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu.
Rais Rouhani ameyasema hayo katika mazungumzo yake na mabalozi wapya wa Iran katika nchi za Senegal, Thailand, the Ufilipino, Ubelgiji, Pakistan, Denmark, Ugiriki, Sri Lanka na Malaysia. Amesema kuwa kipaumbele kikuu cha Iran ni kusaidia juhudi za kuwepo mshikamano na udugu katika ulimwengu wa Kiislamu na kuongeza kuwa, Tehran inalipa umuhimu mkubwa suala la kustawishwa uhusiano na nchi za Kiislamu.
Ametilia mkazo udharura wa kutumiwa vyema fursa iliyopatikana baada ya kutiwa saini makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1 kwa ajili ya kupanua zaidi uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni na nchi mbalimbali.
Vilevile Rais Hassan Rouhani ameitaja Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa inashika bendera ya mapambano halisi dhidi ya ugaidi.
Tarehe 14 Julai mwaka huu Iran na nchi za kundi la 5+1 ambazo ni Marekani, Uingereza, Ufaransa, Russia, China na Ujerumani zilitia saini makubaliano ya nyuklia ambayo yanatazamiwa kufunga faili la nyuklia lililokuwa likitumiwa na nchi za Magharibi kama kisingizio cha kuiwekea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu.

3460023

Kishikizo: rouhani iran kiislamu umoja
captcha