IQNA

Ugaidi

Kundi la kigaidi la Daesh ladai kuhusika na hujuma Moscow iliyoua watu 115

16:39 - March 23, 2024
Habari ID: 3478562
IQNA-Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) limedai kuhusika na hujuma ya kigaidi ambaye imepelekea watu wasiopunua 115 kupoteza maisha Moscow, mji mkuu wa Russia,

Taarifa iliyotumwa kwenye mtandao wa Telegram Daesh imedia kwamba wapiganaji wake walishambulia mkusanyiko mkubwa nje kidogo ya ­­­­­­­Moscow, na kwamba wamerejea kwenye ngome zao salama.

Ikulu ya Rais wa Russia, Kremlin, imetangaza habari ya kukamatwa watu 11, wakiwemo wanne waliohusika moja kwa moja katika shambulio hilo lililolenga jumba la tamasha mjini Moscow jana Ijumaa, na kuua makumi ya watu.

Kremlin imesema kuwa Huduma ya Usalama ya Shirikisho inafanya kazi kubaini upande ulioshirikiana na magaidi waliofanya shambulio hilo.

Kamati ya Uchunguzi ya Russia imetangaza mapema leo Jumamosi, ikinukuu data za awali, kwamba kwa uchache watu 115 waliuawa katika shambulio hilo, na kuonya kwamba idadi ya waliouawa huenda ikaongezeka.

Kamati hiyo imesema, washukiwa hao wamekamatwa katika eneo la Bryansk la Russia, karibu na mpaka wa Ukraine.

Idara ya Usalama ya Urusi imesema washukiwa wa shambulio hilo walipanga kuvuka mpaka na walikuwa wakiwasiliana na watu wengine upande wa Ukraine.

Shirika la habari la TASS limemnukuu Katibu wa Baraza la Usalama la Russia , Nikolai Patrushev, mshirika mashuhuri wa Rais Vladimir Putin, akisema leo kwamba waliohusika na shambulio la tamasha karibu na Moscow wataadhibiwa.

Patrushev ameongeza kuwa: "Shambulio hilo limeonyesha kiwango cha tishio la ugaidi kwa Russia."

Katika ngazi ya kimataifa, Umoja wa Mataifa umeeleza kusikitishwa kwake na shambulio hilo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan'ani amesema kuwa, shambulio hilo la kinyama nchini Russia kwa mara nyingine tena limeonyesha kuwa, ugaidi na uchupaji mipaka ni tishio kwa ulimwengu mzima.

Video iliyosambaa mitandaoni inaonyesha watu wanne waliojizatiti kwa bunduki ya otomatiki wakiwamiminia risasi watu waliokuwa wamekusanyika kwenye ukumbi wa tamasha kwenye viunga vya mji wa Moscow, dakika dakika chache baada ya kujiri mripuko na moto mkubwa kusambaa ukumbini hapo.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump katika kampeni zake za kuwania urais aliwahi kusema kuwa kundi la kigaidi la Daesh liliasisiwa na rais wa zamani wa nchi hiyo Barack Obama. Kundi hilo limehusika na vitendo vya kigaidi na kuua maelfu ya watu wasio na hatia duniani kote. Serikali ya Russia imekuwa mstari wa mbele kupambana na magaidi wa Daesh nchini Syria na imeweza kufanikiwa kuwaangamiza magaidi hao katika nchi hiyo ya Kiarabu.

3487696

Habari zinazohusiana
captcha