IQNA

Mauritania yaandaa Kongamano la Kimataifa la Qur'ani

14:08 - December 22, 2015
Habari ID: 3468305
Mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott ni mwenyeji wa kongamano la kimataifa kuhusu namna mafundisho ya Qur'ani yanavyoweza kuwasaidia Waislamu.

Kongamano hilo  ambalo limefanyika chini ya anwani ya "Kutekeleza Mafundisho ya Qur'ani na Nafasi yake katika Kutatua Matatizo ya Ummah wa Kiislamu", limeanza Jumatatu 21 Desemba.
Kuna washiriki kutoka Morocco, Tunisia, Senegal, Turkey, Niger, Saudi Arabia na Gambia.
Kongamano hilo limeandaliwa na Jumuiya ya Utamaduni wa Kiislamu Mauritania na Afrika Magharibi katika fremu ya mpango wa 'Kumhami Mtume Muhammad SAW'. Hafla hii hufanyika kila mwaka mwezi wa Rabi ul Awwal katika kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad SAW yaani Miladun Nabi.


Akihutubu katika ufunguzi wa kongamano hilo, Waziri wa Elimu Mauritani ameashiria hadhi ya Mtume Muhammad SAW na kusisitiza kuwa mahaba kwa Mtume yanapaswa kubainishwa katika kutekeleza madundisho ya Qur'ani na Mtume SAW.
Aidha amewapongeza walioandaa hafla hiyo kwa jitihada zao za kustawisha mafundisho ya Mtume SAW.

3468092

 

captcha