IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Sudan Yakamilika

16:22 - January 12, 2016
Habari ID: 3470034
Awamu ya 7 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Sudan yamekamilika.
Mashindano ya Kimataifa  ya Qur'ani Sudan Yakamilika

Mashindano hayo yajulikanayo kama 'Zawadi ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Khartoum ' yalikamilika Januari 10. Kwa mujibu wa Ahmed Hashim Ahmed , mwanachama mwandamizi wa kamati andalizi ya mashindano hayo, sherehe ya kufunga mashindano hayo ya Qur'ani itafanyika Januari 13 katika uukumbi wa Al Sidaqa mjini Khartoum ambapo rais wa nchi hiyo Omar Hassan al Bashir atashiriki.

Amesema mashindano hayo yalifanyika katika kategoria tatu ambazo ni kuhifadhi Qur'ani kikamilifu pamoja na tafsiri ya Juzu 24 kwa wanaume, kuhifadhi Qur'ani kikamilifu kwa wanawake, na kuhifadhi Juzuu tatu za Qur'ani kwa washiriki kutoka nchi zisizo za Kiislamu.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yalikuwa na washiriki kutoka nchi 50 pamoja na wakiwemo wanawake walioshiriki kutoka nchi 21. Pembizoni mwa mashindano hayo washiriki walitembelea vituo vya Qur'ani mjini Khartoum na maeneo mengine ya Sudan.

3466434

captcha