
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo maalumu ya wenye umri wa chini ya miaka 15 yatarushwa moja kwa moja kupitia kanali ya televisheni ya satalaiti ya Shuruq TV.
Ridhwan Hassan mtayarishaji maarufu wa vipindi vya kidini katika televisheni nchini Algeria ambaye hivi sasa anatayarisa kipindi cha kila wiki cha "Mazamir Dawood" katika kanali ya Shuruqh TV, hivi sasa ameanza kazi za mradi mpya wake wenye anuani ya Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya "Mazamir Dawood".
Tarehe ya kufanyika mashindano hayo ya kitaifa ya Qur'ani itatangazwa baadaye. "Mazamir Dawood" ni Zaburi au nyimbo tukufu za Dawood AS. Zabur ni jina la kitabu ambacho kwa mujibu wa riwaya za Kiislamu, kilimteremkia Dawood, mmoja wa mitume wa Bani Israil. Zaburi asili iko lwa lugha ya Kiibrania na imejaa dua na minong'ono na Mola Muumba sambamba na kumsifu. Kitabu hicho kiliteremshwa baada ya Taurati.