IQNA

Waislamu Uingereza wapindukia milioni tatu kwa mara ya kwanza

14:56 - February 03, 2016
1
Habari ID: 3470111
Idadi ya Waislamu Uingereza kwa mara ya kwanza wamepindukia milioni tatu kwa mara ya kwanza huku nusu yao wakiwa wamezaliwa nje ya nchi hiyo.

Idadi ya Waislamu Uingereza imeongezeka mara mbili katika kipindi cha muongo moja uliopita kutokana na uhamiaji na kiwango cha juu cha watoto wanaozaliwa.

Katika baadhi ya maeneo ya London, takribani nusu ya wakaazi wote ni Waislamu, imesema Ofisi ya Takwimi za Kitaifa.

Iwapo mkondo huu utaendelea, maeneo kadhaa ya London yatakuwa ni yenye idadi kubwa ya Waislamu kuliko wafuasi wa dini nyinginezo katika kipindi cha miaka 10.

Aidha takwimu zainaonyesha kuwa Waislamu katika maeneo ya England na Wales nchini Uingereza walizaliwa nje ya nchi hiyo huku kila moja kati ya wanne akiwa na umri wa chini ya miaka 10 jambo ambalo linaashiria kiwango kikubwa cha watoto wanaozaliwa katika jamii ya Waislamu.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, kuna Mwislamu katika kila watu 20 Uingereza.

Idadi kubwa zaidi ya Waislamu katika eneo moja ni katika mtaa wa Hamlets, Mashariki wa London ambapo Waislami ni asilimia 45.6 ya wakaazi wake wote na kufuatia na mtaa jirani wa Newham ambapo Waislami wanakadiriwa kuwa asilimia 40.8. Nje ya London idadi kubwa ya Waislamu walio katika eneo moja imeripotiwa katika mji wa Blackburn, kaunti ya Lancashire, ambapo wanakadiriw akuwa asilimia 29.1 ya wakaazi wote wa mji huo. Miji ya Slough na Luton pia imetajwa kuwa ambayo Waislamu ni robo ya idadi ya wakaazi wote huku miji ya Birmingham na Leicester nayo pia ikiwa na idadi kubwa ya Waislamu.

Idadi ya Waislamu Uingereza inatazamiwa kuongezeka kwa kasi kutokana na wahajiri wengi ambao wameingia nchini humo kutoka Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika kipindi cha mwaka moja uliopita.

3458948

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Abdullah Masakata
0
0
Amaa kweli uislam ni dini inayokua kwa kasi,hakika watu wanaendelea kuslimu makundi kwa makundi.
captcha