IQNA

12:17 - January 23, 2022
Habari ID: 3474840
TEHRAN (IQNA)- Kituo cha zamani cha polisi katika mji wa Cardiff eneo la Wales nchini Uingereza kitabadilishwa kuwa msikiti.

Kituo cha polisi cha Old Police Station mtaa wa St Mellons kilibadilishwa kuwa makao ya muda ya Kituo cha Waislamu Cardiff Mashariki tokea mwaka 2019 na mwkaa jana kuliwasilishwa pendekezo la kubomoa jengo hilo na kujenga jengo la kisasa la kudumu.

Pendekezo hilo sasa limeidhinishwa na Manispaa ya Cardiff na shughuli ya kubomoa itaanza baadaye mwaka huu.

Kuna mpango wa kujenga kituo kikubwa ambacho kitajumuisha msikiti, ukumbi wa mikutano ya kijamii na shule ya Kiislamu.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamepinga ujenzi wa msikiti katika eneo hilo kwa kisingizo kuwa kutakuwa na msongamano mkubwa wa magari. Hatahivyo waliowengi katika eneo hilo wanasema kituo cha Kiislamu kutakuwa na athari chanya katika jamii.

Mji wa Cardiff una baadhi ya jamii kongwe zaidi za Waislamu nchini Uingereza ambao wametoka maeneo mbali mbali duniani. Kwa mujibu wa sense ya mwaka 2011. Kuna Waislamu 45,000 eneo la Wales na karibu nusu yao wanaishi mjini Cardiff.

3477486

Kishikizo: msikiti ، cardiff ، wales ، uingereza ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: