IQNA

Waislamu Uingereza

Mchango mkubwa kwa ajili ya ujenzi mpya wa Msikiti wa Blackburn

15:24 - October 09, 2022
Habari ID: 3475903
TEHRAN (IQNA) –Pauni za Uingereza 24,000 zilikusanywa kwa ajili ya ujenzi wa moja ya misikiti mikongwe zaidi huko Blackburn nchini Uingereza.

Tukio hilo katika Masjid-e-Rizwan katika Mtaa wa Newton lilipongezwa kwa mafanikio makubwa na waandaaji ambao walisema £24,000 zilichangishwa na washiriki 2,000 ili kusaidia katika ukarabati.

Asif Naik, rais wa Masjid-E-Rizwan, alisema: "Huu ni wakati wenye kubakia katika  kumbukumbu katika Masjid-E-Rizwan, ambapo kila mtu alikusanyika katika jamii zikiwemo shule na biashara.

"Kila mtu alifurahia chakula, shughuli na mkusanyiko wa kijamii, na ilikuwa ya kushangaza kuona watoto wengi wakifurahia.

"Fedha zilizopatikana zilikuwa za kushangaza, lakini mafanikio makubwa hapa ni jinsi jamii ilivyokusanyika kusaidia na kufurahiya."

Mwalimu Mkuu, Miss Arshad aliandamana na watoto wanane kutoka shule ya msingi wa St. Thomas iliyo karibu kusaidia kuchangisha na kuendesha vibanda.

Bibi Arshad alisema: "Asante kwa Bw. Naik na timu kwa kuwashirikisha watoto wetu katika hafla ya jamii kuchangisha pesa kwa ajili ya mradi wa msikiti.

“Siku hiyo ilikuwa ya mafanikio makubwa, ilileta watu kutoka jamii mbalimbali pamoja kusherehekea siku hiyo ya furaha ya familia. Asante kutoka kwa kila mtu katika St. Thomas."

Mnamo 2019, wadhamini wa Jumuiya ya Waislamu wa Kokni walipewa ruhusa ya kujenga upya na kupanua msikiti.

Gharama ya makadirio ya ukarabati huo inasemekana kuwa zaidi ya Pauni 800,000, iliyofadhiliwa na michango ya kibinafsi, na msikiti huo mpya utachukua waumini 450.

3480778

captcha