IQNA

Waislamu Uingereza

Wafadhili waahidi Pauni 126,000 kusaidia Msikiti Mpya huko Blackburn

21:53 - March 10, 2023
Habari ID: 3476687
TEHRAN (IQNA) – Tukio la kuchangisha fedha kusaidia kujenga msikiti mpya wa Blackburn nchini Uingereza limefanikiwa sana baada ya wafadhili kuahidi kwa ukarimu £126,000 kusaidia mradi huo.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, wafanyakazi wa kujitolea wamekuwa wakifanya safari za hisani na kuendeshaji baiskeli safari ndefu ili kuchangisha fedha za kujenga msikiti huo mpya.

Kituo kipya cha Elimu ya Kiislamu, ambacho kinajumuisha msikiti, kitaandaa matukio ambayo yatalenga kushughulikia masuala kama vile afya ya akili, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na uhalifu.

Misikiti ni moyo wa jumuiya za Kiislamu na unasimama kama mfano halisi wa imani ya Kiislamu.

Msikiti unatumika kwa ajili ya sala za kila siku na sala ya Ijumaa, hafla za mwezi mtukufu zaidi wa Kiislamu, Ramadhani, kama vituo vya elimu na habari, na pia kama mahali pa ustawi wa jamii.

3482752

Idadi ya Waislamu imeongezeka kutoka asilimia 4.9 hadi asilimia 6.5 katika muongo mmoja uliopita nchini Uingereza kulingana na sensa iliyotolewa Novemba 2022.

Sensa hiyo mpya, iliyotolewa na Ofisi ya Takwimu za Kitaifa (ONS), iligundua kuwa idadi ya watu wanaojitambulisha kuwa Waislamu imeongezeka kwa milioni 1.2 katika miaka 10, na kufanya idadi ya Waislamu kufikia milioni 3.9 mnamo 2021.

3482752

captcha