
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Qur’ani hizo za dijitali zimetolewa na Wizara ya Awqaf ya Kuwait na Taasisi ya Taslim ya Malaysia.
Nakala hizo za Qur’ani Tukufu zenye sauti katika muundo wa dijitali zimezawadiwa wenye ulemavu wa machi pembizoni mwa Maonyesho ya 22 ya Vitabu mjini Casablanca.
Imad al Matwa, Mkurugenzi wa Taaissi ya Al Manbir inayofungamna na Wizara ya Awqaf imesema nakala hizo za Qur’ani katika muundo wa dijitali zitawawezesha wenye ulemavu wa macho kusoma na kuhifadhi Qur’ani.
Kila nakala iliyozawadiwa inagharibu dila 120.
Badr Al Aqeel Al Azimi, Mkurugenzi wa Kamati ya Utamaduni katika Wizara ya Aqwaf Kuwati amesema zawadi hizo ni katika sehemu ya miradi ya pamoja ya Kuwait na Morocco.
Maonyesho ya 22 ya Vitabu Casablanca yalianza Februari 12 na yataendelea hadi Februari 21.