IQNA

Khitma ya Sheikh Ghalwash yafanyika Tehran

16:54 - February 18, 2016
Habari ID: 3470145
Khitma ya marhum qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Ragheb Mustafa Ghalwash imefanyika mjini Tehran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, khitam hiyo ilifanyika Jumanne katika ukumbi wa kidini wa Husseinya Zahra SA na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wanaharakati na maafisa wa Iran katika uga wa Qur'ani pamoja.

Kati ya waliohudhuria ni mwenyekiti wa Baraza Kuu la Qur'ani Iran Ali Moqaddam, naibu mwenyekiti wa baraza hilo Seyed Ali Sarabi, naibu mkurugenzi wa kanali ya televisheni ya Qur'ani Iran Mojtaba Izadi, mkurugenzi wa Idhaa ya Qur'ani Iran Mohammad Hussein Mohammadzadeh pamoja na maustadh bingwa wa Qur'ani kama vile Sadrzadeh, Imamjuma, Bonyadi na Qasirzadeh.

Khitma hiyo ilianza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu ya Habibullah Pourahmadi, Mehdi Adeli na Jafar Fardi.

Baada ya hapo hadhirina walisikiliza kanda ya video ya qiraa ya Sheikh Ghalwash pamoja na harakati zake za Qur'ani na safari alizowahi kufanya katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sheikh Mustafa Ghalwash aliyekuwa qarii katika Radio ya Qur'ani ya Misri na mwanachama wa Jumuiya ya Wasomaji (quraa) na Waliohifadhi (huffadh) Qur'ani Misri aliaga dunia na kurejea kwa Mola wake mapema Alhamisi alfajiri Februari 4 akiwa na umri wa miaka 77 katika moja ya hospitali za Misri.
3476272
captcha