IQNA

Mashindano ya Qur'an Tukufu nchini Guyana

14:42 - March 12, 2016
Habari ID: 3470192
Mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur'an Tukufu yamefanyika nchini Guyana (Amerika ya Latini) kwa kushiriki watu 38 katika daraja tofauti.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mashindao hayo yaliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Georgetown yameandaliwa na taasisi ya jamii ya Kiislamu kwa kushirikiana na taasisi ya kimataifa ya kuhifadhi Qur'an kupitia kongamano la kimataifa nchini humo.

Kamati ya uratibu wa mashindano hayo yaliyokuwa na duru nne imesema kuwa, sherehe za kuhitimisha mashindano hayo zilihudhuriwa na Ustadh Faisal Firuz, mkuu wa taasisi ya Kiislamu nchini Guyana, Sheikh Abdul-Alim Rahim, mkuu wa taasisi ya jamii ya Kiislamu nchini humo na wawakilishi wa taasisi na jumuiya za Kiislamu za nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Aidha Wasomi mbalimbali wa Qur'an kutoka maeneo tofauti ya nchi hiyo wamehudhuria duru ya mwisho ya mashindano hayo.

Msemaji wa mahafali hayo amesisitizia umuhimu wa kuhifandhi Qur'an Tukufu na kuwataka wazazi kuwahimiza watoto wao kukienzi Kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu ambacho ndio turathi adhimu ya Waislamu duniani.

3482544

Kishikizo: guyana
captcha