IQNA

Kuhani wa Kizayuni ataka kila asiye Myahudi afukuzwe Palestina

22:57 - April 09, 2016
Habari ID: 3470237
Viongozi waandamizi wa utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel wamezidi kuonesha ukatili wao baada ya kushindwa kukabiliana na Intifadha ya Quds
Katika tukio la karibuni kabisa, kuhani mmoja mwandamiza wa Kizayuni ametaka kila asiye Myahudi afukuzwe Palestina.

Televisheni ya al Alam imemnukuu mtaalamu mmoja wa utawala wa Kizayuni akisema katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa na kanali ya kumi ya televisheni ya utawala wa Kizayuni kwamba, kuhani huyo maarufu wa Israel anayejulikana kwa jina la Ovadia Yosef ametoa matamshi makali dhidi ya Wapalestina kwa kusema kuwa, ni haramu kwa kila asiye Myahudi (yaani Wapalestina) kuweko katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Kuhani huyo mkubwa wa utawala wa Kizayuni ameongeza kuwa, jeshi la Israel linapaswa kutumia nguvu zake zote kukandamiza Intifadha ya Quds.

Maneno hayo ya kichochezi yanayoonesha chuki kubwa waliyo nayo viongozi wakubwa wa kidini wa utawala wa Kizayuni, yametolewa katika hali ambayo, mara kwa mara walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakivamia na kufanya ukatili katika maeneo ya Wapalestina, bali hata katika Masjidul Aqsa, Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Ikumbukwe kuwa hadi hivi sasa karibu Wapalestina 210 wameshauawa shahidi na maelfu ya wengine kujeruhiwa tangu ilipoanza Intifadha ya Quds mwezi Oktoba, 2015.

3486998/

captcha