Qur'an Tukufu, bila shaka, inawatofautisha Mayahudi kati na wanaoamini Siku ya Kiyama na wale Mayahudi wanaovunja ahadi zao.
"… Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno." (Aya ya 66 ya Surah Al-Ma’idah)
Qur’ani Tukufu inataja sifa nyingi mbaya kwa kundi la pili katika historia na zinaweza kugawanywa katika makundi ya kidini, kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Kundi la kwanza linajumuisha baadhi ya tabia sifa mbovu kama vile uasi na kutomtii Mungu, kupotosha amri na dhana za Mungu katika Taurati, mwelekeo wa uchawi, ukafiri, kukataa amri za Mwenyezi Mungu na manabii, kuua manabii wa Mwenyezi Mungu, na uadui na Mwenyezi Mungu na malaika.
Vile vile kuna sifa nyingine mbaya katika kundi hili kama vile kukataa mwongozo wa Mwenyezi Mungu, kushindana katika kutenda madhambi, kujidai kuwa wao ni watu wa Mwenyezi Mungu na kutopata adhabu yoyote katika jamii yao, kuficha mafundisho ya Mwenyezi Mungu, kushindwa kuifanyia kazi Taurati , kuwaamrisha wengine kufanya wema na hali ya kuwa wanashindwa kufanya wema wao wenyewe, na kumsahau Mwenyezi Mungu na Akhera.
Kundi la pili la sifa mbaya za Mayahudi, ambalo ni la sifa mbaya za kijamii, linajumuisha hadi sifa hasi kama vile ubaguzi wa rangi, kueneza ufisadi, kuwa na moyo mgumu kama mwamba, uadui dhidi ya Waislamu, daima kutafuta visingizio na kutoa visingizio, ukaidi, unafiki na ubadhirifu.
Ama zile sifa mbaya za kiuchumi za Mayahudi, Qur’ani Tukufu inazitaja sifa hizo kuwa ni ubakhili, riba, wizi na kupenda anasa za kidunia.
Baadhi ya sifa mbaya za kisiasa za Mayahudi ni kama vile kupenda kuanzisha vita, uhaini, kuvunja ahadi, dhulma na ukandamizaji, kujaribu kuwadhuru Waislamu, kujaribu kuharibu dini na nuru ya Mwenyezi Mungu duniani, kueneza mifarakano na migongano, ujasusi , fitna na ugaidi.
Katika utafiti kuhusu sifa mbaya zilizotajwa katika Qur’ani Tukufu kuhusu baadhi ya Mayahudi, tunaweza kusema kwamba sifa mbaya za Mayahudi katika zama zetu zinahusiana na Mayahudi ambao ni Wazayuni ambao wameunda utawala wa Kizayuni wa Israel. La kusikitisha ni kuwa baadhi ya watawala wa nchi za Kiislamu wanatafutilia sera ya kuanzisha na utawala huo wa Kizayuni huku wakipuuza husiano maonyo ya Qur'ani Tukufu kuhusu pote hilo la Mayahudi.
3488550