IQNA

Mayahudi Katika Qur'ani /6

Watu wenye tamaa na pupa kwa mujibu wa Qur'ani

17:16 - August 08, 2024
Habari ID: 3479244
IQNA – Qur’ani Tukufu inawataja Mayahudi kuwa ni watu wenye pupa zaidi ya maisha ya kidunia na wanaelezewa kuwa wenye pupa na tamaa zaidi kuliko Mushrikeen (washirikina). Ikumbukwe kwamba Qur'ani Tukufu ina misimamo miwili juu ya Mayahudi. Moja ni kuhusu wale Mayahudi wanaomwamini Mungu Mmoja na Siku ya Kiyama na wakatenda mema na wao ni miongoni mwa “Watu wa Kitabu”.

Kundi jingine ni wale Mayahudi wasiomuamini Mwenyezi Mungu na Ufufuo na wanaopanga njama dhidi ya Uislamu. Kwa hakika, hawa ni Mayahudi waliotajwa katika Aya zinazozungumzia sifa mbaya za watu wa Kiyahudi.

Kundi la pili la Wayahudi walikuwa wachoyo na wenye pupa sana huku manabii wengi wakiwa wametumwa kwao na wangeweza kutumia mafundisho na ushauri wao ili waokolewa kutoka njia ya upotofu.

Ikielezea kundi hili la Mayahudi, Qur’ani Tukufu inasema: “Na hakika utawaona ni wenye kuwashinda watu wote kwa pupa ya kuishi, na kuliko washirikina. Kila mmoja wao anatamani lau angeli pewa umri wa miaka elfu. Wala hayo ya kuzidishiwa umri hayamuondoshei adhabu; na Mwenyezi Mungu anayaona wanayo yatenda.” (Aya ya 96 ya Surah Al-Baqarah)

Kwa mujibu wa aya hii, Mayahudi hawa ndio watu wenye pupa zaidi ya maisha ya dunia kwani wanadhani maisha marefu yanaweza kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Moja ya sababu za kiwango hicho cha pupa na uchoyo miongoni mwa kundi hili la Mayahudi inaweza kuwa ni ukosefu wao wa imani ya kweli ya akhera. Qur'ani Tukufu  inasema: “Enyi mlio amini! Msiwafanye rafiki zenu watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia. Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera, kama makafiri walivyo wakatia tamaa watu wa makaburini." (Aya ya 13 ya Surah Al-Mumtahina)

Ijapokuwa Watu wa Kitabu (Wakristo na Mayahudi) wanaamini Siku ya Kiyama, kundi hili la pili la Mayahudi liko chini ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na halina matumaini ya malipo ya Akhera. Ndiyo maana hali yao si tofauti na ile ya makafiri.

Aya hii inawakumbusha waumini juu ya laana ya milele ya kundi la pili la Wayahudi, ili waepuke urafiki na maingiliano nao.

3488535

Kishikizo: qurani tukufu mayahudi
captcha