Taarifa kutoka kwa familia ya sheikh huyo zinasema askari wa utawala huo wamemtia mbaroni kwa kile walichosema ni kusalisha Sala hiyo bila kupewa kibali cha kufanya hivyo. Askari hao wasioheshimu sheria za dini ya Kiislamu pia wamemtuhumu pia Sheikh Muhammad al-Mansi kuwa ametoa hotuba ya kidini bila ya ruhusa.
Inafaa kukumbusha hapa kwamba mienendo ya kuwatia mbaroni masheikh na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Bahrain ni sehemu ya siasa ambazo zimekuwa zikitekelezwa mara kwa mara na utawala huo wa kurithishana nchini Bahrain. Utawala huo unatekeleza siasa hizo za ukandamizaji kwa lengo la kuzima mapambano ya wananchi wa nchi hiyo dhidi ya dhulma na madikteta wa taifa hilo.
Hadi sasa maelfu ya wanaharakati na viongozi wa kidini akiwemo Sheik Ali Salman, Katibu Mkuu wa harakati ya Kiislamu ya Al-Wifaq, wanaendelea kushikiliwa katika korokoro za utawala huo wa Bahrain mbele ya kimya cha jamii ya kimataifa. Hata hivyo na pamoja na ukandamizaji huo, maandamano dhidi ya utawala huo yameendelea kushuhudiwa katika maeneo tofauti ya utawala huo kibaraka wa Saudi Arabia.