IQNA

Siku ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yafana

17:49 - May 13, 2016
Habari ID: 3470309
Alhamisi ilikuwa siku ya kwanza ya Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran ambapo washiriki 16 waliweza kuonyesha ustadi wao katika kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano ya siku hiyo yalianza kwa qiraa ya Mehdi Gholamnejad ambaye alikuwa mgeni mwalikwa.

Kisha maqarii 8 na mahufadh 8 kutoka nchi mbali mbali walipanda jukwaa katika siku hiyo ya kwanza.

Wawakilishi wa Iraq, Jamhuri ya Azerbaijan, Pakistan, Bangladesh, Morocco, Ufilipino, Iran na Indonesia walishindana katika kategoria ya qiraa usiku wa kwanza.

Katika kategoria ya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu, walioshindano walikuwa ni kutoka Bangladesh, Pakistan, Egypt, Morocco, Australia, Tanzania na Ethiopia.

Halikadhalika katika siku hiyo ya kwanza kulikuwana hafla maalumu ya kuenzi familia za mashahidi.

Halikadhalika wananchi Wairani wa matabaka mbali mbali walihudhuria mashindano hayo.

Aidha washiriki wenye ulemavu wa macho pia nao wana kitengo maalumu katika mashindano ya mwaka huu.

Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalizinduliwa rasmi Jumatano usiku katika Ukumbi Mkubwa wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran.

Nchi zaidi ya 70 zimetuma wawakilishi katika Mashidano ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo yanaanza wik hii, Tehran mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kuna washiriki 130 katika mashindano hayo ambayo kaulimbiu yake ni "Kitabu Kimoja Umma Moja”.

Picha za Mashindano ya Qur'ani

Siku ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yafanaSiku ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yafanaSiku ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yafanaSiku ya kwanza ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yafana

/3497431

captcha