IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yaanza Tehran

10:32 - May 12, 2016
Habari ID: 3470306
Mashidano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yameanza Jumatano usiku mjini Tehran.
Mashidano hayo yamefunguliwa rasmi katika Ukumbi Mkubwa wa Sala (Musalla) wa Imam Khomeini MA, na kuhudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu Iran akiwemo Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, Ali Larijani.

Mashindano hayo yalianza kwa qiraa ya Aya za Qur'ani Tukufu iliyosomwa na Ustadh Jawad Panahi na kisha baada ya hapo, Hujjatul Islam Ali Mohammadi Mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran alihutubu katika kikao hicho. Katika hotuba yake , Sheikh Mohammadi aliwakaribisha washiriki wa kigeni na kumshukuru Mwenyezi Mungu SWT kwa fursa ambayo Iran imepata kuwakirimu wageni kutoka nchi zaidi ya 70 duniani.

Amesema mashindano ya Qur'ani husaidia kuleta mazingira mazuri ya kueneza utamaduni wa Qur'ani Iran na kote katika ulimwengu wa Kiislamu.

Aidha amesisitiza kuwa mashindano ya mwaka huu yanafanyika kwa msingi wa kuimarisha umoja wa Kiislamu na kwa msingi huo kaulimbiu ya mashindano ya 33 ni "Kitabu Kimoja, Umma Moja."

Kwingineko Sheikh Mohammadi aliashiria kuwepo harakati nyinginezo pambizoni mwa mashindano hayo ya Qur'ani na kuashiria moja ya harakati hizo ambayo ni Kongamano la 7 la Kuwaenzi Wanawake Watafiti wa Qur'ani.

Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo ya Qur'ani, Spika wa Bunge la Iran Ali Larijani amesisitiza kuhusu umuhimu wa kusoma na kutafakari kuhusu Qur'ani na kutekeleza mafundisho yake.

Mashindano hayo yatakuwa katika kategoria mbili ambazo ni qiraa na kuhifadhi Qur'ani kikamilifu. Aidha kutakuwa na kategoria maalumu ya qiraa kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa macho.

Mashindano ya mwaka huu ya Qur'ani yana majaji 17 wakiwemo kutoka Iran na pia wengine kutoka Iraq, Pakistan, Indonesia, Syria na Yemen.

Hapa chini tizama picha za baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Qur'ani Tehran mwaka huu

3497239

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yaanza Tehran

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yaanza Tehran

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yaanza Tehran

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yaanza Tehran
Kishikizo: mashindano iqna
captcha