Nchi 74 zitatuma wawakilishi katika Mashidano ya Kimataifa ya Qur'ani ambayo yanaanza wik hii, Tehran mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam wal Muslimin Ali Mohammadi Mwakilishi wa Faqihi Mtawala
na Mkuu wa Shirika la Awqaf la Iran. Akizungumza na waandishi habari
Jumatatu mjini Tehran, amesema kutakuwa na washiriki 130 kutoka nchi 75
katika Mashindano ya 33 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran.Ameongeza kuwa mashindano hayo yatakuwa na washiriki 57 katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na wengine 57 katika kategoria ya qiraa. Aidha amesema mwaka huu kutakuwa kitengo maalumu cha washiriki 16 wenye ulemavu wa macho.
Sheikh Mohammadi amebaini kuwa mashindano ya mwaka huu yatakuwa na majaji 10 wa kigeni na 8 kutoka Iran.