IQNA

Uchunguzi wa Maoni

Wananchi Uingereza, Marekani waunga mkono kususiwa Utawala wa Kizayuni wa Israel

13:46 - June 01, 2016
Habari ID: 3470351
Zaidi ya thuluthi moja ya Wamarekani na karibu nusu ya wananchi wa Uingereza wanaunga mkono kususiwa na kuwekewa vikwazo utawala wa kizayuni wa Israel.

Utafiti wa maoni uliofanywa na shirika la kimataifa la Ipsos umenyesha kuwa, asilimia 40 ya Waingereza na asilimia 33 wa Marekani wanaunga mkono kikamilifu kususiwa utawala haramu wa Israel chini ya Harakati ya Kimataifa ya Kuisusia Israel BDS.

Duru za habari zimearifu kuwa, harakati ya BDS imeshika kasi duniani na hata miongoni mwa wasomi wa Israel, huku ripoti iliyotolewa mwezi uliopita ikionyesha kuwa, maprofesa mashuhuri wa Israel wanaunga mkono na hata kuhimiza watu wa matabaka mbali mbali kuususia utawala haramu wa Israel.

Hii ni katika hali ambayo, aasisi 16 za kimataifa kote ulimwenguni zimelaani kitendo cha utawala wa Kizayuni wa Israel cha kumpiga marufuku ya kusafiri, Omar Barghouthi, mwasisi wa Harakati ya Kimataifa ya Kuisusia Israel BDS. Harakati ya Kimataifa ya Kuisusia Israel BDS inaungwa mkono na jumuiya mbalimbali za kijamii, makundi ya kidini, taasisi zisizo za kiserikali na tawala za wananchi katika kona mbalimbali za dunia, na kila leo uungaji mkono huo. 

3459975
captcha