Katika ujumbe wake kwa viongozi wa nchi za Kiislamu kwa munasaba wa
kuwadia mwezi mtukufu wa Ramadhani, Rais Hassan Rouhani amewataka
viongozi wa nchi hizo kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa dunia
ni pahala salama.
Amesema : "Katika kipindi hiki muhimu kwa historia ya Uislamu, taswira ya kuogofya na bandia ya Uislamu inatishia turathi za kihistoria, falsafa na udugu wa wafuasi wa dini hii tukufu."
Rais Hassan Rouhani amesisitiza kuwa, kuna haja kwa Waislamu wote
kuarifisha taswira halisi na sahihi ya Uislamu na kuudhihirishia
ulimwengu kuwa Uislamu ni dini ya amani, huruma na inayohimiza
ushirikiano na mshikamano. Rais Rouhani katika ujumbe wake huo ameongeza kuwa, mwezi huu mtukufu wa Ramadhani unatoa fursa na kipindi cha kuunga na
kuimarisha udugu miongoni mwa Waislamu. Rais wa Iran ametoa mkono wa kheri na
fanaka kwa viongozi wa nchi za Kiislamu, serikali na Waislamu wote kwa munasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani