IQNA

Maonyesho ya Istanbul kuhusu 'Vitu 1001' vilivyovumbuliwa na Waislamu

22:57 - July 04, 2016
Habari ID: 3470431
Chuo Kikuu cha Biruni huko Istanbul Uturiki kimeandaa maonesho kuhusu 'Vitu 1001 vilivyovumbuliwa na Waislamu duniani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maoneysho hayo yanaonyesha namna wanasayansi na wasomi Waislamu walivyotoa mchango mkubwa katika elimu na sayansi duniani kwa kuvumbua vitu vingi sana katika kipindi cha miaka 1000 ambayo inatajwa kuwa 'zama za dhahabu' katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Maonyesho hayo yanaoneysha mchango mkubwa wa Waislamu katika taalamu za hisabati, fizikia, afya, tiba, sayansi, utamaduni n.k.

Maoneysho hayo yataendelea hadi Agosti 15 na yanafanyika kwa msingi wa kitabu cha Profesa Salim al Hassani, mhadhiri wa uhandisi ambaye ameandika kitabu cha 'Uvumbuzi vya Vitu 1001'. Maonyesho hayo tayari yameshafanyika katika miji ya London, New York, Paris, Beijing na Kuala Lumpur.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Will Durant mwanahistoria wa Kimarekani amezungumzia kasi ya ukuaji wa elimu kutokana na athari ya mafundisho ya Mtume wa Uislamu, Muhammad al Mustafa SAW. Kuhusiana na nukta hiyo anasema:"Ustaarabu wa Uislamu ulifikia kwenye kilele cha ustawi na maendeleo katika anuai za elimu na fani za ufundi kuanzia mwaka 81 hadi 598 Hijria sawa na mwaka 700 hadi 1200 Miladia. Elimu za amali na tajiriba zikiwemo za utabibu, kemia, fizikia, jiolojia, biolojia na botania zilifikia kilele cha ustawi, ambapo wanasayansi na wavumbuzi wakubwa kabisa walioenea katika Ulimwengu wa Kiislamu walikuwa wakisomesha, wakiandika na kufanya utafiti katika elimu hizo. Wao walifanya kazi ya kuzifikisha na kuzifunza elimu hizo kuu za msingi kwa majirani na watafutaji wa elimu katika nchi mbalimbali... Will Durant anaendelea kuandika:" Katika kipindi cha kung'ara kwa Uislamu ulimwengu wa Magharibi ulikuwa umezongwa na fikra za Zama za Kati (Middle Ages), ushenzi na mgando wa kifikra wa Kanisa, na kuwa mbali kikamilifu na utumiaji akili na utaalamu wa ufundi. Na kinyume chake katika Ulimwengu wa Kiislamu kulikuwepo wataalamu wa kupigiwa mfano kama vile Ibn Sinaa, Kharazmi, Farabi, Muhammad bin Zakariyya Razi, Abu Raihan Biruni, Hakim Omar Khayyam, Ibn Khaldun na wengineo ambao walikuwa wakishughulika na uenezaji elimu duniani bila ya mpaka wala kizuizi chochote."

3512807

Kishikizo: waislamu uvumbuzi iqna
captcha