Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Kadinali Ranjith ameyasema hayo Ijumaa katika mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo alipokutana na kufanya mazungumzo na Seyyed Hassan Khomeini, mkujuu wa muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini MA.
Kadinali huyo ameashiria nafasi ya Imam Khomeini katika kustawisha maadili ya mwanadamu na kusema moja ya mafanikio makubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kuhuisha thamani takatifu za Mwenyezi Mungu katika jamii.
Ameongeza kuwa, Uislamu na Ukristo ni dini ambazo zinapaswa kushirikiana na kuhakikisha kunaeneza thamani takatifu za Mwenyezi Mungu duniani.
Kadinali wa Sri Lanka pia ameashiria masaibu ya watu wa Palestina na kutaja hatua ya Israel kukalia kwa mabavu ardhi za Palestina kuwa aibu kwa jamii ya mwanadamu. Amesisitiza umuhimu wa Wapalestina kurejeshewa haki zao ili amani ipatikane duniani.