IQNA

Mabomu ya Saudia yaua Waislamu 160 katika mazishi nchini Yemen

10:16 - October 09, 2016
Habari ID: 3470606
Raia wasiopungua 160 wameuawa kinyama katika mji mkuu wa Yemen Sana'a baada ya ndege za kijeshi za Saudi Arabia kuwashambulia walipokuwa katika kikao cha mazishi.

Katika tukio hilo la kusikitisha la jana Jumamosi Alasiri,ndege za kivita za Saudia zilitekeleza mashambulio kadhaa  dhidi ya waombolezaji Waislamu waliokuwa katika shughuli ya mazishi mjini Sana'a.

Duru nchini zinasema watu 160 wameuawa kwa umati katika shambulio hilo la ndege za kijeshi za Saudia. Ripoti zaidi zinasema kuwa, miongoni mwa waliouawa wapo maafisa wa ngazi za juu wa serikali ya Yemen.

Aidha watu zaidi ya  500 wanaripotiwa kujeruhiwa katika jinai hiyo huku kukiweko na uwezekano wa idadi ya vifo kuongezeka. Hujuma hiyo ya kinyama ya  Saudia dhidi ya waombolezaji imetajwa kuwa ni mauaji ya umati.

Tangu ulipoanzisha uvamizi wake wa kijeshi dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka uliopita, hadi sasa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na utawala wa Aal Saud na kuungwa mkono na Marekani na Israel umeshazishambulia skuli, hospitali, makaazi ya raia misikiti, barabara, masoko na kambi za wakimbizi na kuua maelfu ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo. Zaidi ya watu 10,000 wamepoteza maisha katika hujuma ya kinyama ya Saudia dhidi ya Yemen.

 Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amelaani vikali mauaji yaliyotekelezwa jana na Saudia dhidi ya raia wasio na hatia Yemen. Akizungumza katika usiku wa saba wa maombolezo ya Muharram, Nasrallah amesema jinai ya Jumamosi Alasiri ya utawala wa Saudia huko San'aa  ni jinai ya kuogofya. Aidha amesema si jambo la kushangaza kuona Saudia ikitekeleza jinai kama hivyo.

 Kwingineko vyama vya kisiasa Yemen vimelaani vikali ukatili huo wa Saudia na kutaka jamii ya kimataifa ichukue hatua za kivitendo dhidi ya ukoo wa Aal Saud. Mohammad Al Bakhiti mmoja wa viongozi wa harakati ya Ansarullah  ya Yemen amesema jinai hiyo ya Saudia itapelekea kuingia duru mpya ya mapambano ya watu wa Yemen dhidi ya Saudia.

 3461122

captcha