IQNA

17:03 - December 31, 2019
News ID: 3472321
TEHRAN (IQNA) – Idara ya Kufuatia Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika Chuo cha Al Azhar nchini Misri imelaani hatua mwanasiasa mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi ya kupanga kufanyika mashindano ya vibonzo vya kumdhalilisha Mtume Muhammad SAW.

Katika taarifa, idara hiyo imesema mpango huo unalenda kuumiza hisia za Waislamu Uholanzi na dunia nzima sambamba na kueneza chuki na ubaguzi.

Geert Wilders, mwanasiasa mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi sambamba na kutoa mwaliko, ametaka kufanyika mashindano ya vibonzo vya kumdhalilisha Mtume Muhammad SAW kwa lengo la kujeruhi hisia za Waislamu.

Wilders ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter akitaka kufanyika mashindano hayo ya vibonzo kumhusu Mtume wa Uislamu SAW. Mwaka jana mwanasiasa huyo mwenye chuki dhidi ya Uislamu nchini Uholanzi na kutokana na mashinikizo yaliyotokana na malalamiko ya kupinga mashindano ya vibonzo vyenye kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW alilazimika kulegeza msimamo na kuvunja mashindano hayo.

Idara ya Kufuatia  Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika Chuo cha Al Azhar imesema Wilders hapaswi kutumia kisingizio cha uhuru wa maoni na kuongeza kuwa, kuheshimu matukufu ya kidini si ukiukwaji wa uhuru wa maoni.

Aidha idara hiyo imetoa wito kwa serikali na taasisi za kimataifa kuchukua hatua za kuzuzi kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu.

3867832

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: