IQNA

Qarii wa Misri, Sheikh Radhi, aaga dunia + Video ya Qiraa

23:59 - December 10, 2016
Habari ID: 3470733
IQNA-Qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Abdul Wahid Zaki Radhi ameaga dunia Ijumaa akiwa na umri wa miaka 80.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Radhi alikuwa qarii mashuhuri duniani ambaye alifanikiwa kutembelea zaidi ya nchi 30 duniani kwa ajili ya kusoma Qur’ani Tukufu.

Alizaliwa Julai mwaka 1936 katika kijiji cha Shibramnet, mkoa wa Giza nchini Misri. Abdul Wahid Zaki Radhi alihimizwa na wazazi wake kusoma Qur’ani Tukufu akiwa na umri mdogo na akapata taufiki ya kuhifadhi Qur’ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 9.

Alijifunza qiraa ya Qur’ani Tukufu akiwa na maqarii wengine wa eneo hilo kama vile Sheikh Seyed Mustafa Limoun na Sheikh Abdul Hamid Ghali. Baada ya kupata mafunzo kutoka kwa maustadhi wake, aliwezi kuwa qarii mashuhuri katika jimbo lote la Giza.

Mnamo mwaka 1975 Sheikh Radhi alianza kusoma Qur’ani kama qarii rasmi ya radio ya kitaifa ya Misri, katika vikao rasmi vya serikali, katika Swala ya Ijumaa na kwingineko. Tokea mwaka wa 1987 Sheikh Radhi aliteuliwa kuwa qarii rasmi katika Msikiti wa Salaheddin mjini Cairo hadi kifo chake.

Kwa mujibu wa mmoja kati ya marafiki zake, Sheikh Radhi alikuwa akisikiliza sana qiraa cha qarii mwenzake bingwa wa Misri, marehemu Mustafa Ismail.

Bonyeza hapa kusikiliza au kutazama video ya qiraa ya marhum Sheikh Radhi akisoma Qur’ani katika Msikiti wa Al Azhar mjini Cairo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka uliopita wa 1437 Hijria Qamari. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amghufurie na amjaalie pepo.

3552378

captcha