Amesema: Kwa mara nyingine
tunapenda kusisitiza kwamba, ni jambo lililo wazi kuwa, kama mwaliko huo
utatolewa na mazingira yakawa yanaruhusu, basi suala la kutumwa mahujaji
litashughulikiwa na taasisi husika na vyombo hivyo ndivyo vitakavyochukua
maamuzi.
Siku chache
zilizopita kulikuwa na taarifa kuwa, Wizara ya Hija ya Saudi Arabia imezitumia
barua nchi 80 duniani ikiwemo Iran kuzialika kushiriki katika mjadala wa
kufanikisha ibada ya Hija mwaka huu.
Gazeti la al Hayat
linalochapishwa London limeandika kuwa Waziri wa Hija wa Saudia Mohammed Bentin
imeanza mazungumzo na zaidi ya nchi 80, ikiwemo Iran, kuhusu mipango ya Ibada ya
Hija mwaka 2017.Gazeti hilo limeandika kuwa, 'ujumbe wa Iran umealikwa Saudia
kwa ajili ya mazungumzo.'Maafisa wa Iran hadi sasa hawajatoa tamko lolote kuhusu
ripoti hiyo.
Hata hivyo Taasisi ya Hija
na Ziara ya Iran imesema, haijapokea barua yoyote kutoka kwa Wizara ya Hija ya
Saudi Arabia.
Itakumbukwa kuwa
Septemba 2015, kulitokea msongamano mkubwa wa Mahujaji wakati wa Ibada ya Hija
huko Mina karibu na Makka. Saudia ilidai kuwa wau 770 walipoteza maisha katika
msongamano huo. Hatahivyo Iran ilitangaza kuwa Mahujaji 4,700, wakiwemo Wairani
465 walipoteza maisha katika tukio hilo. Kabla ya hapo pia mahujaji wengine 100
walipoteza maisha, wakiwem Wairani 11 wakati winchi ilipoanguka katika Masjidul
Haram.
Kufuatia matukio
hayo, Iran ilitaka usalama wa Mahujaji udhaminiwe lakini Saudia ilikataa
kushirkiana katika suala hilo na hatimaye wakuu wa Saudia wakawazuia mahujaji
Wairani kutekeleza ibada ya Hija mwaka 2016.
Watawala wa Saudia
wanaluamiwa kwa usimamizi mbovu wa Ibada ya Hija jambo ambalo limepelekea idadi
kubwa ya mahujaji kupoteza maisha kila mwaka.
Waislamu duniani
wamekuwa wakitaka utawala wa Saudia uzishirikishe nchi zenye idadi kubwa ya
mahujaji katika usimamizi wa Ibada ya Hija ambayo ni nguzu muhimu ya
Uislamu.
Mkuu wa Shirika la
Hija la Iran mwezi Septemba alisema ni jambo lisilokubalika kwa Saudia kuwauzia
Wairani kuhiji hasa kwa kuzingatia kuwa kuna Wairani ambao wako katika orodha ya
kusubiri Kuhiji miaka 15 hadi 20 ijayo. Ameongeza kuwa, Saudia inaamini kuwa
miji mitakatifu ya Makka na Madina ni milki yake katika hali ambayo maeneo hayo
matakatifu ni milki ya Waislamu wote.